DARASA 01: BILA SHAKA DHIKRI NAMBA MOJA NI QURAN YENYEWE

BILA SHAKA DHIKRI NAMBA MOJA NI QURAN YENYEWE. 


Hadith:

1. Abu Said radhiallahu anhu amesimulia kuwa Rasulullahi amesimulia ktk hadithi Qudsi kuwa Allah anasema; Yule ambaye hawezi kufanya dhikri nyingine na dua kwa sababu ya kushughulishwa na Quran nitampa yaliyo bora zaidi kuliko niliyowapa waombaji wengine na *utukufu wa maneno ya Allah kuliko maneno mengine yote ni kama utukufu wa Allah dhidi ya viumbe vyake vyote*


2. Abuu Dharri ghifari radhiallahu anhu amesimulia kuwa Rasulullahi.... amesema *Hakuna kitu ambacho kinarahisisha kuwa karibu na Allah bora zaidi ya kilichotoka kwake moja kwa moja nayo ni Quran.*


3.Mtume amesema Allah ana watu wake miongoni mwa watu." Maswahaba wakauliza: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni nani hao?” Yeye

akajibu: “Hao ni watu wa *Qur’an* : watu

ya Mwenyezi Mungu na watu wake wateule.” (Ibn Majah)


Na Uthman ibn Affan anatoa testimony (ushuhuda) kuhusu kila mtu kujijua kama kweli yeye MchaMungu kuhusu hili, anasema : *"Kama nafsi zenu zingekuwa zimetakasika, msingelichoka kusoma Quran."* (Kitāb al-Zuhd of Imām Ahmad )


Katika hili la Quran nimalize kwa kusema tu kuwa:


"Usomaji wa Qur-aan ni heshima ambayo Allah

Ameitoa kwa wanadamu. Malaika hawakupewa

heshima hii, na hivyo wana shauku ya kuisikia ikisomwa na

wanadamu.” (Ibn al-Salah)


Usione haya kujifunza Quran ktk ujana au utuuzima wako, pambania ndoto zako, dunia isikufanye umsahau Allah, mbona yeye hatusahau kakupa macho waona, kakupa masikio wasikia ,ona ulivyo mzuri pengine Huna hata kidonda mwili mzima, Leo mpaka vipofu wanahifadhi Quran, tuna nini sisi !!!!!!!! Basi na tuazimie , muda bora kabisa wa kusoma Quran zaidi na kichwa kikakamata ni asubuhi so anza taratibu Leo. Kwa ushauri zaidi waeza tutafuta inbox.


Wako walimu wengi wakike, kwa wakiume, siku za mbele tutakuja kuweka fadhila za sura mbalimbali ukisoma unapata nini. Njaa, watoto, kazi yako, furaha , utulivu, heshima zote utazipata kupitia Quran, tena yapendeza tushindane ktk hili jambo la Quran. Allah atuwezeshe wote, amin amin amin


Daraja Ya juu ya utamu wa Quran ni kuyatafakari maudhui yake sio kusoma tu, jitahidi tujifunze aya za quran ziliteremshwa kutokana na matukio gani, tuisome kana kwamba tunamuona Allah mbele yetu, kama hatumuoni yeye atuona.